Wednesday, 16 July 2014

KIJANA USIKATE TAMAA JIAMINI KWANI UNAWEZA:GAZUKO

Kijana anayefanya vizuri kwenye anga la muziki wa injili kwa sasa kupitia aina ya muziki wake anaoufanya wa kipekee maarufu kwa jina la gospel hip hop huyu si mwingine bali anafahamika kwa jina la Gazuko.

Gazuko ameona ni vema akazungumza na vijana wenzake ambao wengi wao wapo majumbani na wengine wapo katika shule na vyuo mbali huku wakitarajia kuajiriwa pindi wamalizapo masomo lakini Gazuko ameamua kutoa ushauri kwa vijana hao kwamba badala ya kutegemea kuajiriwa ni bora wakawazia kujiajiri kutokana na vipaji walivyo patiwa na Mwenye Mungu kuwa ni talanta...

"unajua Mungu ametupatia sisi wanadamu vipaji tofauti tofauti ambavyo kila mmoja akisimama kwa nafasi yake anaweza kufanikiwa katika maisha yake lakini shida iliyopo kwa vijana wengi huwa wanakabiliwa na roho ya kukata tamaa pindi wanapokutana
na changamoto ndogo na kujikuta wanahama katika vipaji vyao...ebu jaribu kufikiria ingetokea Hasheem Thabit angekata tamaa kwenye mpira wa kikapu na kusema kuwa hapa nyumbani Tanzania hakuna kijana aliyefanikiwa kupitia mchezo huo je leo hii angekuwa na maisha anayoyaishi ? hivyo mimi nina washauri vijana wenzangu tusimame kwenye vipaji vyetu ili tutimize ndoto zetu na kipaji sio lazima uwe msaniii wa kuimba ama kuigiza tu hapana unaweza kuwa una kipaji hata cha kuchonga vinyago au wewe unakawa una kipaji cha kufanya usafi kupitia kipaji hiko cha usafi unaweza ukafungua ofisi ya inayohusihana na mambo ya usafi" Amesema Gazuko ambaye sasa hivi anatamba na video yake ya Acha kulia anayopatikana kwenye youtube.

No comments:

Post a Comment