Monday, 9 December 2013

UNAMFAHAMU PASTOR CHRIS OYAKHILOME?

Amezaliwa katika familia ya kikristo,Alizaliwa tarehe 7 desemba 1962.aliokoka akiwa na miaka 9 na akaanza huduma akiwa bado ni kijana.na kufanikiwa kuongoza makongamano makubwa ya uponyaji akiwa bado yupo shule ya msingi na secondary.amesoma chuo kiitwacho Bendel State University,ambacho kwa sasa kinajulikana kama "Ambrose Alli University"hapo alikuwa akisomea Architecture.

                    
Ameoana na Pastor Anita Oyakhilome ambae ni mkurugenzi wa makanisa ya Christ Embassy International,pia anachunga makanisa ya Christ Embassy huko uingereza,Docklands,Woolwich kaskazini na London.wana watoto wawili wa kike
Pastor chris
Pastor chris pamoja na mke wake pia ni waandishi wa vitabu maarufu sana duniani kama vile Utenzi wa uhakika (Rhapsody of Realities),vitabu vingine ni kama vile "How to receive your miracle and retain it?"na promotes Word of Faith theology
Mafundisho yake yanahusu sana juu ya kufanikiwa kwani ndio ahadi ya Mungu juu ya wana walio wake na akiongezea kuwa umasikini na magonjwa ni kinyume cha mpango wa Mungu(warumi 5:3-4)

Umati wa watu
Huduma yake inaongoza mambo mbalimbali kama vile Healing School, Rhapsody of Realities (a daily devotional with global reach), na N.G.O inayoitwa Innercity Missions wna pia ana television tatu za kikristo: LoveWorld TV, LoveWorld SAT na LoveWorld Plus.tena anaongoza Night of Bliss South Africa FNB Stadium huko Johannesburg,na Higher Life Conferences Canada, United States of America,na United Kingdom
Akiwa katika pozi
Akaunti yake ya @PastorChrisLive ina wafuasi zaidi ya million 1.2 Twitter,na anaongoza mtandao wake wa kijamii uitwao Yookos.na ni miongoni mwa watumishi matajiri sana Africa na duniani kwa ujumla.



                                             

akiwa kazini


No comments:

Post a Comment