Thursday, 3 April 2014

HISTORIA YA ROSE MUHANDO

 LEO KATIKA WASIFU
Leo katika wasifu tunae Rose Muhando,Fahamu Mengi usiyoyajua Kuhusu yeye.

Anaitwa Rose Muhando;amezaliwa mwaka 1976 katika kijiji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro.

Chanzo cha kubadili dini,hapo mwanzo alikuwa ni mwimbaji mzuri sana wa kaswida,na alihudhuria kila siku madrasa huko Dumila morogoro. Baadaye afya yake ilianza kudhoofu kutokana na ugonjwa ambaoa aliangaika kuupima ni ugonjwa gani lakini hakukutwa na tatizo,hali hii ilipelekea maisha kuwa magumu sana.Ndipo alipo amua kwenda kanisani kwenye maombi.baada ya maombi hayo, alipona na hapo ndipo alipoamua rasmi kubadili dini akiwa na umri wa miaka 12. 
Kilichotokea,Baada ya kubadili dini wazazi wake walichukizwa na uamuzi wake,hivyo wakaona ni busara kumfukuza nyumbani kabisa,Hali iliyozidi kuhatarisha maisha yake na kuendelea kutangatanga na kumsababisha aangukie mikononi mwa wanaume ambao alizaa nao watoto. 

Akiwa na mtoto wa miezi sita jijini arusha aliwahi kufukuzwa na mchungaji kisa
alimwomba fedha ili aweze kuingia studio kurekodi.kwa kipindi hicho mtoto alikuwa anaumwa ugonjwa wa pumu na alienda arusha ili aweze kurekodi wimbo wake wa kwanza. 

Alianza muziki rasmi katika kwaya iliyopo Dodoma, baadaye akawa mwalimu wa kwaya hiyo ya Dodoma St. Mary’s katika Kanisa la Kianglikana la Chimuli. aliendelea hivyo mpaka alipoamua kuanza kutunga nyimbo zake mwenyewe kwa msaada wa mfuko wa kwaya yao,

Januari mwaka 2005,alipokea tuzo mbalimbali ikiwamo ya Mtunzi Bora wa nyimbo za Injili, Mwimbaji Bora na Albamu Bora ya Mwaka, zilizotolewa na Tanzania Gospel Music Awards 2004,kupitia albam yake ya Mteule uwe macho

Albamu zake ni pamoja na:
1.Kitimutimu.
2.Uwe Macho, 2004.
3.Jipange Sawasawa, 2008.
4.utamu wa yesu ,2011
5,Yesu kun’guta, ambayo ilitoka januari 2014 
Katika Albam ya Jipange sawasawa
 Kwa sasa rose muhando amesaini mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya Sony Music Africa ya Afrika Kusini alioanza kuutumikia mwaka huu 2014.

No comments:

Post a Comment