Thursday, 28 August 2014

ALICHOSEMA MAINDA KUHUSIANA NA MADAI YA KUGOMBANA KANISANI

Gazeti moja la udaku leo limeandika habari yenye kichwa (MAINDA AGOMBANA KANISANI)
Hiki ndicho alichosema mainda kuhusiana na madai hayo
"Katika maisha ya mwanadamu lazima uwe na siku tatu za mapito.siku zote unapotaka kuanzisha jambo au kufanya kitu wengi hukutia moyo hiyo ndio inakuwa siku ya kwanza.Siku ya pili hii ndio hatari maana hii mimi ninaiita HATARI YA SIKU YA PILI:Mara nyingi mafanikio huwa yanakuja siku ya pili na hapo ndipo watu wale waliokuwa wakikutia moyo wanageuka kuwa maadui usipo kuwa  makini kujisimamia unaweza kupoteza MAONO Yako na hata ukajikuta ukafia hapo,maono uliokuwa nayo na usivuke kwenda siku ya 3 yako.ila ukifanikiwa kwenye majaribu yote ukavuka hiyo namba 2 jua namba 3 wewe ni mshindi.Kuna muda siwezi kuwalaumu waandishi kwa maana wao wako kazini na wala siyo madai zangu nawapenda sana na ninawaheshimu ,ila kuna watu ambao ndio wanaokuzunguka unawaona ni wema kumbe ni mbwa mwitu amejivika ngozi ya kondoo ivi mtu unaanzaje kumpigia mwandishi simu na kumchafua mwenzio bila kosa lolote.Hii najua ni namba mbili yangu ya maisha na nitaivuka tu.SINA LA KUMJIBU MTU MUNGU ANANITOSHA KUNIJIBIA."

No comments:

Post a Comment