Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam ni kampuni maarufu kwa uandaaji wa matamasha ya injili nchini,ikiwa chini ya Mkurugenzi Alex Msama.,kwa sasa ipo katika maandalizi ya nguvu ya Tamasha la kimataifa la muziki wa Injili la Pasaka litakalofanyika kwa mara ya 14 tangu lianzishwe.Tamasha hilo litazinduliwa Aprili 20 katika Uwanja wa Taifa kabla ya kuhamia mikoani.
Hawa ndio Waimbaji waliothibitisha kuwepo katika tamasha la mwaka huu 2014.
1. Rebecca (Afrika Kusini)Itakuwa ni mara ya pili kwake kuja nchini kutumbuiza katika tamasha hilo kwani mara ya kwanza kuja nchini ilikuwa Aprili 6, 2012 kwa kazi ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka la Aprili 8, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam
2. Keke (Afrika Kusini)Mbali ya Malope, safari hii kutakuwa na mwimbaji mwingine kutoka nchini humo ambaye ni Kekeletso Phoofolo ‘Keke’ anayetamba na vibao vyake kibao vyenye mvuto wa aina yake kama ‘Sefapaanong Ke Boha.
3. Faraja Ntaboba (DR Congo),Huyu ni mwimbaji wa kimataifa kutoka DR Congo atakayepamba tamasha hilo, akitamba na vibao mbalimbali ikiwemo albamu yake mpya iliyobebwa na jina la ‘Naomba Niseme na Wewe.,na pia kama utakumbuka alitamba sana nyimbo kama ‘Yupo Mungu’ na Mke wa Pili’
4. Sara Kierie (Kenya),Sara Kierie ‘Sarah K’ ni mwimbaji mahiri kutoka Kenya ambaye ametamba na vibao vingi vilivyotikisa nchini Kenya na Afrika Mashariki, kikiwemo cha ‘Liseme,Mnyunyizi na zingine nyingi
5. Sekeleti (Zambia)Sekereti amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa muziki wa Injili wa Tanzania, kutokana na ubora wa kazi zake pia upendo wa mwamuzi huyo kwa Watanzania hadi kutunga vibao kadhaa vya Kiswahili kama ‘Uniongoze,’ Baraka Zako’ na ‘Huu Mwaka’ na sasa akitesa na albamu ya ‘Vigelegele.’
6. Rose MuhandoMara zote amekuwa
akishiriki tamasha hili tangu mwaka 2000, ni wazi amekuwa sehemu ya tamasha hilo la kimataifa, akichangia kulipatia umaarufu tamasha hilo katika kutimiza malengo yake.
7. Upendo NkoneNyota wengine ni Upendo Nkone ambaye amekuwa baraka kwa wapenzi na mashabiki wa muziki wa Injili kutokana na kushiriki kwake mara nyingi matamasha ya Msama Promotions, yaani Pasaka na Krismasi.
8. Upendo Kilahiro
Upendo Kilahiro naye yu miongoni mwa waimbaji mahiri akiwa na uzoefu mkubwa wa kushiriki matukio ya kimataifa ya muziki wa Injili ambaye amekuwa akihudumu pia nchini Afrika Kusini Na kwa sasa amekuwa ni miongoni mwa waimbaji maarufu wa kuimba Live
9.john lisuHuyu ni mtaalam wa kuimba live na ni mara nyingi amekuwa akishiriki matamasha haya.
10.Bony mwaitege na waimbaji wengine wengi toka hapa Tanzania
No comments:
Post a Comment